Kanisa moja la Berlin Ujerumani limefungua milango kwa Waislamu kusali kwenye kanisa hilo baada ya Misikiti kufungwa kwenye mji huo ili kudhibiti corona.
Padri wa Kanisa hilo amesema “Tunaichukua Ramadan kama kitu chenye maana sana, tunafikiri sala na kukaribishana kila mmoja na hata kwa Mungu ni jambo linalosaidia kusisitiza ubinadamu na amani”
Ingawa madhehebu yamekubaliwa kufunguliwa na Serikali, jumla ya Waumini 50 ndio wanakubaliwa kuingia kusali kwa wakati mmoja lakini kwa Kanisa hili sababu ni kubwa likakubaliwa Watu 100 ndio wakaamua
kutoa nafasi kwa Waislamu ambao misikiti yao ilikua imejaa. (📹 via DW Kiswahili)
No comments:
Post a Comment