Tuesday 11 February 2020

Idadi ya waliofariki kutokana na CoronaVirus nchini China imeongezeka



Idadi ya waliofariki kutokana na CoronaVirus nchini China imeongezeka na kufikia 1,016, huku ikidaiwa kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo kuongezeka.

Imeripotiwa kuwa Vifo hivyo vya Februari 10, vimetokea Hubei (108) na Wuhan (67) ambapo ndio chimbuko la Virusi hivyo
-
Maambukizi mapya 2,478 yamethibitishwa na kuongeza idadi ya walioambukizwa kuwa 42,683
-
Wakati huo huo, viongozi wawili wa juu wa Tume ya Afya katika Jimbo la Hubei wamefukuzwa kazi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!