Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa unaosababishwa na 'corona virus' huko wihan nchini china ambao umeripotiwa kusababisha vifo vya mamia ya watu nchi nyingi zimeonekana kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wa raia wao waishio maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa huo.
Licha ya juhudi zinazofanywa na wazazi wa wanafunzi Watanzania walioko maeneo ya Wuhan ambako ndiko chimbiko la mlipuko huo kuwarejesha nyumbani, Serikali ya Tanzania imeonekana kuchukua hatua kwa speed ya kinyonga hali inayozua sintofahamu miongoni mwa wanafunzi Watanzania walioko Wuhan.
Kwa maelezo ya mwanafunzi mmoja aliyeko Jianghan University hapo Wuhan amesema kuwa wazazi wao wameandika barua mara kadhaa kwa serikali na pia wao wameshafanya kikao na balozi lakini bado serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana na kurejeshwa kwao.
Mwanafunzi huyo pia alisema kutokana na hali kuwa mbaya zaidi hosptali zimefurika wagonjwa mpaka kufikia hatua ya kulaza wagonjwa chuoni hapo.
Nichukue fursa hii kuitaka serikali uchukue hatua za haraka ili kuhakikisha usalama wa Watanzania walioko Wuhan.
JMF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment