Sunday 26 January 2020

WATANZANIA WATAHADHARISHWA!

Wizara ya Afya imesema mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala Mshukiwa wa ugonjwa wa homa ya mafua makali inayosabishwa na kirusi kipya (Corona),hata hivyo kutokana na mwingiliano wa kibiashara na kijamii kati yetu na Nchi nyingine kama China, Tanzania inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo “Wizara imechukua tahadhari kukabiliana na tishio la ugonjwa huo”


“Tunatoa tahadhari kwa Watanzania hususani wanaosafiri kwenda Mataifa yaliyoathirika na mlipuko wa ugonjwa huo unaosababishwa na Virusi vya Corona na wanaopokea Wageni kutoka Nchi hizo kuzidisha makini” -WIZARA YA AFYA
“Dalili za ugonjwa huu unaosababishwa na Corona ni homa na mafua makali, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, kuathirika mapafu, kupumua kwa shida hata kifo, ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, Watanzania wachukue tahadhari”-WIZARA YA AFYA
“Watanzania wachukue hatua ili kujikinga na Virusi vya Corona kwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa, kukaa mbali na Mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri Nchi zilizokumbwa na mlipuko, kuwahi Vituo vya Afya ukihisi dalili za ugonjwa” - WIZARA YA AFYA
#MillardAyoUPDATES

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!