Msanii Shilole ameendelea kuwekea msisitizo kauli yake ya kugombea ubunge huko kwao Igunga ifikapo mwezi wa kumi ambapo amesema anaisubiria kwa hamu siku hiyo ajitokezee kugombea.
Shilole ambaye amefanikiwa zaidi Kwenye shughuli zake za upishi ameendelea mesisitiza kuhamia kwenye ubunge baada ya kuandika kupitia Instagram page yake ikiwa hii siyo mara yake ya kwanza kuongelea swala hili la kugombea.
…>>”Mimi Shishi ambaye ni mbunge kivuli wa mda mrefu wa kujitolea wa jimbo langu la Igunga na ambaye sipo rasmi bungeni kwasasa.
Naisubiria kwa hamu kubwa siku isiyokuwa na tarehe lakini ni mwezi wa kumi jumapili moja hivi asubuhi ya mwaka huu 2020 baada ya ibada ya kwanza, ni siku ambayo nitatangazwa rasmi kama mbunge mwakilishi wa jimbo la Igunga.
Nimefanikiwa kuiweka Igunga kwenye ramani nzuri ya Tanzania bila ya kuwa mbunge rasmi kwahiyo sitashindwa kuifanyia maendeleo Igunga yangu nikiwa mbunge rasmi pale mjengoni.
Wazee na Vijana kwa pamoja nipokeeni kijana wenu nakuja tuiendeleze Igunga. Tukutane Mjengoni, Hapa Kazi Tu.
No comments:
Post a Comment