Tuesday 21 January 2020

Mbwana Ally Samatta rasmi Aston Villa ya England.


Klabu ya Aston Villa imemsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kwa mkataba wa miaka 4 na nusu akitokea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.


Mbwana Ally Samatta amesajili na Aston Villa akitokea KRC Genk ambao ni mabingwa wa Belgium msimu wa 2018/19 ambapo Samatta pia aliibuka mfungaji bora namba mbili.
Miaka 10 iliyopita alikuwa anachezea Simba 2010-2011.

Kuanzia 2011-2016 akachezea TP Mazembe, ambako alishinda Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe Shirikisho pamoja na kuibuka mchezaji bora wa ndani mwaka 2016.
2016 - 2020 akachezea KRC Genk ambako amechukua ubingwa wa Belgium pamoja na Super Cup huku akishiriki UEFA Champions League na Europa League.
Misimu mitatu na nusu ya Samatta ndani ya Genk.
Mechi 191
Magoli 76
Assist 20

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!