Saturday 11 January 2020

Fahumu juu ya ugonjwa wa Gauti(Gout)

Ugonjwa wa Gauti (Gout): Ni Mojawapo ya Maradhi yanayo tokana na Ukosefu wa elimu ya Lishe.
.
Ugonjwa huu watu wengi wanafahamu kwamba unasababishwa na kula nyama ya Mbuzi, ng'ombe kondoo,kitimoto, kiufupi nyama nyekundu.

.
Kitabu cha sayansi Ya Mapishi kilicho andikwa na @boazmkumbomd kimeeleza kwa Kina Ugonjwa huu na Uhusiano wake na Nyama nyekundu na Sukari na wanga.
.
Gauti husababishwa na Mkusanyiko wa Uric acid ambazo zinakuwa katika mfumo wa chumvi kwenye Jointi. Huenda kukausha ute unaolainisha magoti na kisha magoti yanaanza kusagana,Kuvimba na Kuuma sana (Gout attach).
.
Je Uric acid Hutokana na nini?
Hizi Uric acid hutokana na Mwili unapokuwa una ondoa Seli iliyo maliza muda wake kwa kuteketeza DNA na RNA. Pia kutoka kwenye vyakula kwa kuteketeza DNA na RNA.
.
Kila binadamu huzalisha Uric acid mwilini wakati mwili unajiendesha kiafya hata kama usipokula vyakula ambavyo ni nyanzo vya Uric acid mwilini kama nyama. Huzalisha wakati wa kuteketeza seli zilizopatikana baada ya kumaliza muda yaani apoptosis.
.
Ikisha Tengenezwa hutolewaje mwilini?
Uric acid Hutolewa kwa njia kuu ya Mkojo kupitia Figo. Ina maana Uric acid ikisha zalishwa Figo huitoa nje na hii husaidia Uric acid isiongezeke na isilete madhara mwilini.
.
Je nini Husababisha Uric acid Kuongezeka mwilini?
Kulingana na maelezo hapo juu, Uric acid inaweza kurundikana mwilini kwa Kushuka kwa Utendaji kazi wa Figo. Kwa hio Kitu Chochote kinacho Ipunguzia Figo uwezo wa kuchuja Damu (GFR) basi Kinasababisha Gauti.
.
Ambavyo ni Pombe, Sukari aina ya Fructose (soda na Juisi), Insulin Nyingi damuni (Matumizi ya wanga Kupindukia na Protein powders), Unene/Kitambi, Kisukari, Presha nk
.
Je Nyama Inahusikaje Kwenye Gauti?
Ni sawa na wewe nikuzabe kofi upandishe hasira kwangu akija mwingine akakuchokoza haina maana yeye ndio mwanzilishi wa hasira zako.
.
Nyama, Maharage samaki, mboga za majani matunda vyote vikichakatwa mwilini Utapata DNA na RNA na hatimaye hutengezwa URIC ACID ila kwa sababu Utendaji kazi wa Figo uko Chini Na Uric acid sasa Imerundikana basi UNACHOKOZA HALI HIO ZAIDI ila haina maana Nyama au samaki Inaleta gauti.
.
.
Nyama haina uhusiano wowote wa kushusha utendaji kazi wa Figo zaidi ya sababu nilizo zitaja hapo juu.
.
Ukitaka Kiwango cha Uric acid kishuke vizuri kabisa kwenye damu. Akili yako na Nguvu zako zote zielekeze kwenye KUBORESHA UTENDAJI KAZI WA FIGO kwa sababu asilimia 95 na zaidi watu wengi wanapata GAUTI kwa sababu ya KUSHUKA KWA UWEZO WA FIGO KUCHUJA URIC ACID NJE.
.
.
Gauti sio Ugonjwa wa Masikini ni Ugonjwa Wà Maisha ya Kifalme watu wanao ishi maisha ya kimagharibu, Soda sana Pombe sana, Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari na wanga nk l
KIBAYA ZAIDI NA NDIO SABABU WAGONJWA WENGI HAWAPATI NAFUU.
Unamkuta anakunywa Pombe, soda, Vyakula vya ngano Kila kitu anafukia mijuisi nk Halafu hali nyama anasema inaleta Gauti. Matokeo yake HAJAWAHI KUPATA NAFUU MAISHA YAKE YOTE TANGU ABADILISHE HUO MFUMO WAKE.

Unavyotakiwa Kuacha ndivyo unavyokula. Haipo siku Uric acid Itashuka. Hebu Tekeleza SAYANSI YA MAPISHI

Imeletwa kwenu na Dr. Boaz Mkumbo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!