Wednesday 29 January 2020

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

No photo description available.#Coronaviruses vinavyopatikana zaidi kwa Wanyama, mara machache virusi hivyo vinaweza kuambukizwa kutoka kwa Mnyama kwenda kwa Binadamu
- Huwafanya Watu kuugua katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa na mafua ya kawaida


Virusi husambaa kutoka kwa Binadamu mmoja hadi mwingine kwa njia ya Hewa kwa Kukohoa au Kupiga Chafya, Kugusana na mtu mwenye virusi hivyo

Njia nyingine ni Kugusa Kitu au sehemu yenye virusi na kisha kujigusa mdomo, pua au macho kabla ya kunawa na mara chache huambukiza kupitia kinyesi

Dalili za kuwa umepata virusi hivi ni pamoja na Pua kudondosha mafua mfuulizo, Kuumwa Kichwa, Kukohoa, Kupata homa na muwasho katika Koo ila kwa wenye Kinga ndogo ya Mwili kama Wazee au Watoto wanweza kupata Nimonia(Pneumonia)

Hakuna Kinga ya Virusi hivyo kwa sasa, ila usambaaji wake kwa Binadamu unaweza kupunguzwa kupitia Kuosha mikono yako mara kwa mara kwa maji na sabuni na epuka kugusa macho, mdomo na pua kwa mikono isiyooshwa

Pia, unaweza kupunguza usambazaji wake kwa Kukaa mbali na mtu aliyethibitika kuwa na maambukizi. Ukianza kuona dalili hizo unashauriwa kumuona daktari

Ukithibitika kuwa na maambukizi ya Virusi hivyo, vunika mdomo na pua yako wakati wa kupiga chafya au kukohoa na safisha sehemu au kitu ulichokigusa

====

Kirusi hiki cha Corona, kinaaminika kuwa kilianza katika soko la bidhaa za baharini mwishoni mwa mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa linauza nyama ya porini.

Kirusi hicho kinaweza kusababisha homa, kukohoa, kupumua kwa shida na homa ya mapafu. Kirusi hicho ni sehemu ya familia ya kirusi corona ambacho kinauhusiano na virusi vya SARS na MERS ambavyo vilisababisha milipuko siku za nyuma.

Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, pia katika maeneo mengine duniani kama Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, Malaysia, Vietnam, Taiwan, Singapore, Nepal, Macau, Hong Kong na Canada.

Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kuwa, idadi ya watu wapatao 2045 wamegundulika kuwa na kirusi hiki huku wapatao 633 wakipatikana kwa siku ya jana pekee.

324 kati ya hao 2045 wako katika hali mbaya zaidi (critical condition) huku idadi ya waliokufa kutokana na kirusi hicho ikifikia 56 nchini China.

====

Hapo awali, China ilitoa tahadhari kuwa kirusi hiki kinaweza kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Waziri wa Kamisheni ya Afya ya Taifa nchini China, Ma Xiaowei, akizungumza na vyombo vya habari, alisema kuwa, uwezo wa serikali wa kufahamu kirusi hiki kipya ni finyu na hawajui hatari zinazoweza kuambatana na kubadilika kwa kirusi hiki. [VOA]

Ma Xiaowei alisema muda ambao kirusi hiki cha corona huchukuwa hadi kujitokeza ni kati ya siku mmoja hadi 14, na kuwa kirusi hiki kinaambukiza hata wakati kinajijenga mwilini, kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa homa kali ya mafua, SARS, kirusi corona kilichoibuka China na kuua takribani watu 800 duniani mwaka 2002 na 2003.

Mpaka sasa juhudi zilizokwisha kufanyika ili kudhibiti kuenea kwa kirusi hiki ni pamoja na katazo la usafirishaji na kusafiri na kusitisha matukio ya sherehe kubwa. China imetoa makatazo kadhaa ya kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya sana katika nchi hiyo ili kuzuia kuenea kwa kirusi hicho.

Muendelezo wa haya pamoja na yatakayokuwa yakijiri tutapata kuyafahamu kwa kina.

====

SASISHO: Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona imeongezeka kutoka 106 hadi 131.

Taarifa ya vifo vipya 25 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pamoja na visa vipya takribani 840 kwa siku ya jana pekee (Januari 28).

SASISHO: Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona (Coronavirus) imekwisha fikia 106 hivi sasa kutoka idadi iliyoripotiwa mara ya mwisho ya 82.

Mkoa wa Hubei, China pekee umeripoti visa vipya takribani 1291 na vifo vipya 24.

Wagonjwa wapatao 690 wana hali mbaya zaidi.

SASISHO: Beijing, China imetangaza kifo cha kwanza kabisa katika jiji hilo kutokana na kirusi cha Corona, mwanamume wa miaka 50 aliyekuwa amesafiri kwenda Wuhan tarehe 8, Januari na kurejea jijini Beijing tarehe 15. Idadi ya vifo imefikia 82.

SASISHO: Kifo kingine kimeripotiwa kutokana na kirusi cha Corona katika mkoa wa Hainan nchini China. Hicho ni kifo cha kwanza kabisa katika mkoa huo. Jumla ya vifo kutokana na kirusi hicho ni 81 mpaka sasa.

SASISHO: Idadi ya vifo nchini China kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 80 mpaka sasa huku idadi ya wenye maambukizi ikifikia zaidi ya 2700 ikijumuisha Hong Kong, Macau pamoja na Taiwan.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!