Tuesday 10 December 2019

UGALI WA MTAMA NDIYO UGALI BORA ZAIDI KULIKO UGALI MWINGINE WOWOTE HATA DONA IKASOME UPYA KWA MTAMA


Mtama una virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika mwili wa binadamu.
Tafiti zinaonyesha kuwa mtama una kiasi cha wanga, nishati, nyuzi nyuzi, na mafuta karibu au sawa na mahindi au nafaka nyingine.


Mtama una madini aina ya chuma na chokaa kwa wingi kuliko mahindi au nafaka nyingine.
Una protini kwa wingi kuliko mahindi, mchele au ngano.
Mafuta yake hayana lehemu (kolesto), Una vitamin B complex, vitamin C na vitamin E kwa wingi.
Mtama una madini ya zinki, phosphorus, potassium, na manganese kwa wingi kuliko nafaka nyingine.
Mtama una vimelea viitwavyo phenolica mbavyo ni mhimu sana kwa mwili kujikinga na saratani, Mtama hauna gluten hivyo ni salama kutumiwa na watu wenye matatizo au ugonjwa wa Celiac.
Muhimu: Sukari yake huyeyuka taratibu sana mwilini hivyo mtama ni chakula kinachofaa kuliwa na watu wenye magonjwa kama kisukari.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!