Wednesday, 11 December 2019
Mlishe mtoto wako vyema baada ya miezi sita
Akiwa na umri wa miezi 6, anza kumpa mtoto wako aina nyingine ya vyakula pamoja na kumnyonyesha. Endelea kumnyonyesha hadi atakapotimu umri wa miaka miwili au zaidi.
Baada ya miezi 6 watoto wanahitaji aina nyingine ya vyakula pamoja na maziwa ya mama ili kuwafanya kuendelea kukua vyema. Aina mbali mbali za vyakula vitamsaidia mtoto wako katika njia mbali mbali. Wape watoto wako mchanganyiko wa vyakula hivi mbali mbali kila siku.
Vyakula hivi vinaweza kupikwa kulingana na mahitaji. Baada ya miezi 6 mpe vyakula vya aina mbali mbali kila siku. Mtengee mtoto kijiko na kisahani cha kutumiwa na yeye tu. Mtayarishie uji ambao ni mzito kiasi cha kuweza kukaa kwenye kijiko.
Kila mara, mlishe mtoto uji pamoja na vyakula vingine. Watoto ambao hawatakula vizuri wakati huu huenda wakawa na afya mbaya na wapungufu katika werevu maisha yao yote. k Maharagwe, dengu, nyama, kuku, samaki, na kiiniyai husaidia kujenga mwili wa mtoto wako. k Wali, viazi, ugali, mahindi, mtama, na matoke humpa mtoto wako nguvu. k Matunda na mboga kama vile mboga za majani, karoti, malenge, machungwa, maembe, na mapapai, yatamkinga mtoto wako dhidi ya maradhi
Fuata viwango vilivyopendekezwa:
Baada ya miezi 6 Vijiko vya kula viwili au vitatu kila wakati wa chakula Mara mbili au tatu.
Miezi 7-8 u Nusu ya kikombe kila wakati wa chakula mara tatu kwa siku
Miezi 9-11 u Robo tatu ya kikombe kila wakati wa chakula mara tatu kwa siku
Chakula chepesi kimoja Miezi 12-24 kikombe kimoja kila wakati wa chakula mara tatu kila siku
Chakula chepesi mara mbili kwa siku
Saidia mtoto wako kula lakini usimlazimishe kula. Mwangalie kwa makini, uwe mvumilivu na umpe mda kadri unavyo hitajika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment