Kuna faida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;
■ Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuupatia mwili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari “sucrose” ambayo kazi yake kuu ni
kutengeneza nguvu mwilini. Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa.
■ Ingawa juisi ya miwa ina utamu lakini inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa “Low Glycemic Index”. Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni muhimu pia kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.
■ Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma na manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume “Prostate cancer” na kansa ya maziwa “Breast Canser”
■ Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na kuimarisha ufanyaji kazi wa figo.
■ Juisi ya miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono “STDs” na kidney stones.
■ Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano.
■ Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng’enyo wa chakula.
■ Husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo.
■ Vilevile husaidia katika kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa “constipation”.
■ Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meno kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini.
No comments:
Post a Comment