Wednesday 10 April 2019

Maziwa ya Ng'ombe kwa mtoto


Maziwa ya ng'ombe yamekuwa yakitumika mara nyingi kama chakula cha watoto. Wazazi wengine huwaanzishia maziwa ya ng'ombe mapema sana watoto.



 Wengi wanaanzishia maziwa kwa kuamini kwamba watoto wao hawashibi, wengine ni wale ambao wana sababu za kiafya za kuwafanya washindwe kunyonyesha lakini hawana uwezo wa kununua maziwa maalumu kwa ajili ya watoto.
Licha ya kwamba maziwa ya ng'ombe yamekuwa yakitumika miaka nenda rudi, lakini haipendekezwi kupewa watoto chini ya mwaka mmoja. Kwa mfano chama cha madaktari wa afya ya watoto wa Marekani(AAP) kinapendekeza kwamba "Mtoto chini ya mwaka mmoja asipewe maziwa ya ng'ombe". Endapo utalazamika kumpa mtoto maziwa ya ng'ombe, hakikisha umeyachemsha katika joto la kutosha ili kuuwa vijidudu.
Kwanini mtoto chini ya mwaka mmoja asipewe maziwa ya ng'ombe?
Watoto wadogo wanapotumia maziwa ya ng'ombe:- 1.hawapati kiasi cha kutosha cha madini ya chuma, asidi ya linoleic pamoja na vitamin A.
2.Pia watoto hupata kiasi kikubwa kuliko kiwango kinchachohitajika cha Potasium, Sodium na Protein.
3.Watoto pia hupoteza damu kidogo kidogo kwenye utumbo endapo wanatumia maziwa ya ng'ombe.
Tofauti ya maziwa ya ng'ombe na maziwa ya mama!
Kuna tofauti ya virutubisho vilivyomo katika maziwa ya ng'ombe na yale ya binadamu. Kutokana na tofauti hiyo ndio maana maziwa ya ng'ombe ambayo hayajaboresha hayafai kutumia na mtoto mdogo. Maziwa ya unga ni maziwa ya ng'ombe yaliyoboreshwa kwa kuongezewa virutubisho vya aina mbalimbali.
Zifuatazo ni tofauti kati ya maziwa ya ng'ombe na maziwa ya mama:-
1.Maziwa ya ng'ombe yana kiasi kikubwa cha protein ambayo haifai kutumika
2.Maziwa ya ng'ombe hayana kiasi cha kutosha cha virutubisho vya Taurine na Cysteine.
3.Linoleic acid iki kwa kiwango kidogo kwenye maziwa ya ng'ombe
4.Madini ya Zinc hayachukuliwi kwa urahisi kutoka kwenye maziwa ya ng'ombe
5.Maziwa ya ng'ombe hayana kinga kwa ajili ya mtoto kama yalivyo maziwa ya binadamu.
6.Pia maziwa ya binadamu ya kemikali ambayo husaidia kupunguza uwezo wa bakteria kuzaliana.
Hitimisho: Kama huna sababu yoyote ya kiafya ya kukuzia kunyonyesha, mnyonyeshe mtoto wako kwa muda wa miezi sita. Kama utalazamika kumpa maziwa ya ng'ombe hakikisha maziwa yamechemshwa kwa kiwango kinachotakiwa ili kuuwa bakteria.

1 comment:

Amina said...

Habari. Blog nzuri sana. Tunakukaribisha kukupa ofa ya kuitangaza blog hii kwenye mtandao wetu mkubwa unaokuwa kwa kasi afrika mashariki upo kama facebook. Bonyeza jina langu kuutazama. Unalipia sh 100 tu kwa siku kutangaza tunapokea kuanzia sh elfu 5 tu Karibu uitambulishe blog yako kwa watazania wengi zaidi kwamwaka

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!