Wednesday, 10 April 2019
Rais Magufuli tangu aingie madarakani hajasaini mtu aliyehukumiwa kifo anyongwe
Rais John Magufuli amesema, tangu aingie madarakani hajasaini mtu aliyehukumiwa kifo anyongwe lakini akipelekewa kesi ya mtu aliyeua mtoto atamuomba malaika wake na huenda atasaini.
Rais amesema, anatubu kwa kuongoza watu wanaoua watoto mkoani Njombe na ameongoza sala ya kutubu. Amesema, mauaji ya watoto mkoani humo ni mambo ya kijinga na kwamba mtu hawezi kutajirika kwa kuua watoto. Awali katika mkutano huo wa hadhara alitangaza kumuondoa Mkuu wa Polisi wa Wilaya lakini baada ya sala alitangaza kumsamehe. Rais Magufuli amemshukuru Mungu kwa kusamehe dhambi zilizofanywa mkoani Njombe na sasa mkoa huo ni mpya. Kiongozi huyo wa nchi yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Njombe.
HABARI LEO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment