
Mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo, Ismael Ngaile, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Renatus Zakeo akisoma maelezo ya kesi hiyo ya jinai namba 8/2018, alidai Chora anakabiliwa na kosa la kumbaka mama yake mzazi, Rhobi Nyang'ombe (65) kinyume cha sheria.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha kifungu namba 130 (1) na (2) (e) na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai Desemba 26, 2017 saa 3:00 usiku katika kijiji cha Burunga kata ya Uwanja wa Ndege wilayani hapa, mshtakiwa alimwingilia mama yake bila ridhaa yake, alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada MUG/IR/145/2018.
Awali, Samson alipofikishwa mahakamani hapo alisomewa kosa la kuzini na mama yake.
Hata hivyo, jana Mahakama ilifanya marekebisho katika shauri hilo na la ubakaji baada ya kujiridhisha kuwa alimwingilia kwa nguvu.
Shahidi wa kwanza wa Jamhuri ambaye ni mama yake mshtakiwa alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba Mosi shauri hilo litakapoanza kusikilizwa huku mshtakiwa akirejeshwa mahabusu.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment