hapa ni kile ambacho kitaweza kukupa
nishati lishe (kalori ) yenye theluthi moja
ya nishati lishe inayotakiwa kwa siku ile.
Anza kunywa uji wa dona asubuhi au
kunywa uji wa mtama au ngano ambayo
haikukobolewa sana, kula magimbi,
Muhogo uliochemshwa, au kama kuna
viazi vitamu vile vyenye rangi ya njano
hapo mambo ndipo yatakapo noga.
Ukipata kipande cha tunda la msimu
kama embe, nanasi, tikiti maji, chungwa.
Kwa wale wanaoishi ukanda wa pwani,
uji kwa mafenesi ni chakula kizuri sana
kwa mtoto aendae shuleni asubuhi au
baba au mama aendae shambani au
kwenye ajira yoyote ile. Ukipata karanga
kiasi kidogo tu, mlo wa asubuhi wenye
mkusanyiko huo ndio mlo unakubalika
kiafya.
viazi vitamu vile vyenye rangi ya njano
hapo mambo ndipo yatakapo noga.
Ukipata kipande cha tunda la msimu
kama embe, nanasi, tikiti maji, chungwa.
Kwa wale wanaoishi ukanda wa pwani,
uji kwa mafenesi ni chakula kizuri sana
kwa mtoto aendae shuleni asubuhi au
baba au mama aendae shambani au
kwenye ajira yoyote ile. Ukipata karanga
kiasi kidogo tu, mlo wa asubuhi wenye
mkusanyiko huo ndio mlo unakubalika
kiafya.
Achana na maandazi, chapati au
vitumbua asubuhi vilivyojaa mafuta,
vyakula kama hivyo hunenepesha mwili
na sio vyakula asilia.
Vyakula asilia nilivyovianisha ndivyo
vyenye mlomakapi (fibre) Vyakula vyenye
mlomakapi haviyeyushwi na
kusharabiwa na mwili, bali vinasaidia
kusafisha mabaki ya sumu mbali mbali
(free radicals) na pia husaidia anayekula
vyakula vyenye mlo makapi, mtu huyo
asilani katika uhai wake akiendelea kwa
hatua hizo hataongezeka uzito kiholela,
na pia atajiepusha na kupata saratani ya
utumbo mpana (colon cancer) na
ataweza kujikinga asipate ugonjwa wa
kisukari na shinikizo la damu litapungua
au kutoweka.
Tuwe na saa maalum za kula chakula
cha jioni ili tuweze kupata mlo wa
asubuhi wa kufungua kinywa wenye
theluthi mbili za kalori zote zinazo
hitajika kwa siku moja. Watoto walale
mapema wapigishwe mswaki kabla ya
kulala.
cha jioni ili tuweze kupata mlo wa
asubuhi wa kufungua kinywa wenye
theluthi mbili za kalori zote zinazo
hitajika kwa siku moja. Watoto walale
mapema wapigishwe mswaki kabla ya
kulala.
Asubuhi kunywa maji kama glasi mbili
kuna saidia kusafisha tumbo. Fanya
zoezi kidogo pata mlo wa asubuhi
wenye moto kama uji na viazi vya
kuchemsha magimbi na muhogo kama
ipo matunda kidogo na karanga kama
zipo. Mlo huo pia ni mzuri kwa mtoto
anayekwenda shule. Nishati yetu
inatokana na chakula.
Seli zako katika ubongo hazina sukari ya
kutosha wakati wa asubuhi na huna
hifadhi ya nishati lishe.
Watu wengi huchoka kwa sababu
hawali kifungua kinywa asubuhi.
Wanakacha kifungua kinywa.
No comments:
Post a Comment