Monday 19 March 2018

IGP, DCI na AG waitwa Mahakamani kujibu kuhusu Abdul Nondo

Leo March 19,2018 tunayo story kuhusu Mwanafunzi Abdull Nondo, ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa wito kwa Mkurugenzi wa Upelelezi Tanzania (DCI), Mkuu wa Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani hapo kujibu hoja kuhusu Nondo kutofikishwa mahakamani.


Akizungumza na Ayo, Wakili wa kujitegemea, Jebrah Kambole amesema wamewasilisha maombi kuhusu Nondo katika Mahakama hiyo tangu Ijumaa iliyopita wakiwa na hoja tatu.
Amesema maombi hayo wanaomba apewe dhamana, ama apelekwe mahakamani ama aachiwe huru.
“Tangu aletewe Dar es Salaam hakuna aliyeonana naye si ndugu, mawakili wala wanafunzi wenzake na hajafikishwa mahakamani hivyo tumeona njia ya pekee ni kwenda mahakamani kwa sababu ana haki ya kupata dhamana kama watu wengine,” -Jebrah.
Jebra amesema kuwa kutokana na maombi waliyoyafungua, leo March 19, Mahakama Kuu imetoa wito kwa DCI, IGP na AG ili wafike mahakamani kujibu hoja hizo.
“Mahakama imetoa wito kwa viongozi hao ambapo wametakiwa kufika mahakamani March 21, 2018,” -Jebrah

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!