Sunday, 17 December 2017

Zanzibar: Hatuogopi Kenya hata kama wako nyumbani

Nahodha wa Zanzibar Suleiman Kassim
Image captionNahodha wa Zanzibar Suleiman Kassim
Timu ya Zanzibar imeshangaza wengi kufuzu fainali ya mashindano ya kandanda ya kombe la Senior Challenge itakayofanyika katika uwanja wa Machakos Disemba tarehe 17.

Wapinzani wao kwenye fainali ni wenyeji Kenya ambao wana kocha mpya kutoka Ubelgiji, Paul Put. Kocha huyo ambaye ana mlima wa kupanda dhidi ya Zanzibar walio na uchu wa kushinda kombe hilo kwa mara ya pili.
``Hatuogopi Kenya sisi hata kama wanacheza nyumbani, wembe ni ule ule tuliomnyioa nao Waganda mechi yetu ya nusu-fainali, tutajaribu tupate bao la mapema,`` asema kocha Hemed Suleiman.
Ama kwa hakika Zanzibar imekua gumzo nchini Kenya na Afrika Mashariki na Kati kwa jumla kutokana na matokeo yao mazuri kwenye mashindano haya, kinyume na matarajio ya wengi.
Wamezima miamba ya kandanda eneo hili, Kenya, Tanzania bara na Uganda ambao walimeza mabao 2-1 kwenye mechi ya nusu-fainali, wafungaji wakiwa ni Abdul Azizi Makame na Mohammed Issa Juma huku Derrick Nzibambi akiipatia Uganda bao lao la kufutia machozi.
Walienda sare tasa na Kenya na wakanyoa Tanzania bila maji kwa bao 1-0 kwenye mechi za makundi, kipigo ambacho kiliwaudhi sana wachezaji, wasimamizi na mashabiki nchini Tanzania.
Matokeo haya bora yamewaongezea matumaini chama cha kandanda cha Zanzibar kutambuliwa na shirikisho linalosimamia kandanda duniani, Fifa.
Image captiNahodha wa Zanzibar Suleiman Kassim

Katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee
Image captionKatibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee

Matumaini ya kuwa mwanachama wa FIFA

Kwa miaka mingi wamejaribu bila mafanikio kuwa mwanachama wa Fifa lakini kocha Hemed Suleiman na katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee wana imani hatimaye Fifa itasalimu amri.
``Tumeonyesha dunia nzima tunastahili tuwe wanachama wa Fifa na ushindi wetu, hatahivyo hatuwalazimishi ila ni kwa hiari yao watuorodheshe kama wanachama wao,'' asema kocha Suleiman.
``Hii ni haki yetu sisi Wazanzibari kuwa wanachama. Asiyeona hili basi hana macho,'' asema Khamis Ali, na kuongeza:``Angalia Uingereza na mataifa yake madogo jirani kama Scotland na Ireland ni wanachama pamoja na England. Sasa sisi mbona wametuweka pamoja na Tanzania? Si vibaya maanake hawa ni ndugu zetu, twatumia paspoti moja lakini tunastahili kutambuliwa kivyetu.Hili fungu la Fifa wanalotumia TFF sis hatupati chochote. Ni uwanja tu wa nyasi bandia tumefaidika nao.''
Fifa na shirikisho la Afrika CAF wamekataa kata kata kutambua chama cha kandanda cha Zanzibar kwa kifupi ZFA
Endapo watatwaa kombe hili bila shaka Zanzibar itaendeleza zaidi kampeini yake ya kutambuliwa na Fifa. Lakini baadhi ya wadadisi wa kandanda wanasema haitakua rahisi kushinda Kenya nyumbani.
Kwa jumla Kenya imejikokota kufuzu kwa fainali, na nusra Burundi iwaondoe kwenye nusu-fainali iliyomalizika kwa sare tasa muda wa kawaida ndiposa Whyvonne Isunza akawafungia la pekee na la ushindi wakati wa muda wa ziada.
Zanzibar inacheza mchezo wa kasi na pasi za chini, na ni dhahiri Kenya itatumia nguvu zaidi na mipira mirefu wakitafuta ushindi. Miongoni mwa wachezaji wao wa kutegemewa ni kipa Patrick Matasi, nahodha Musa Mohammed, Jockins Atudo, George ``Bklackberry'' Odhiambo, Isunza, Kefa Aswani na Crispin Oduor Ochieng.
Kwa jumla Kenya imeshinda Senior Challenge mara sita, ikawa ya pili mara saba na ikachukua nafasi ya tatu mara tatu. Na kwa upande wa Zanzibar, mbali na kushinda kombe hilo mwaka wa 1995 walipoilaza wenyeji Uganda bao 1-0 mechi ya fainali, wamemaliza katika nafasi ya tatu mara tatu.

No comments:

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!