Sunday, 17 December 2017

Aliyetoka Jela kwa msamaha wa Rais, Aiba tena na kuhukumiwa miaka 15 Jela


Image result for arrested
Kijana Gerald Deus (30), aliyetoka jela kwa msamaha wa Rais Magufuli, amehukumiwa tena kifungo cha miaka 15 jela kwa tukio la wizi alilolifanya siku ya nne baada ya kuachiwa huru

Deus alihukumiwa kifungo hicho juzi na Mahakama baada ya kukiri kosa la kupora pesa shilingi laki 3 kutoka kwa Dina Mwende, mfanyabiashara wa soda za jumla.

Kwa mujibu wa Hakimu, kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 lakini kutokana na mtuhumiwa kukiri kosa na kutoisumbua mahakama, amepunguziwa adhabu hivyo atatumikia miaka 15 na kazi ngumu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!