Tuesday, 12 December 2017

Oscar Pistorius ajeruhiwa akipigana gerezani

South African paralympian Oscar Pistorius (C) arriving at the Pretoria High Court for sentencing procedures in his murder trial in Pretori
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionOscar Pistorius ajeruhiwa akipigana gerezani
Aliyekuwa mwanariadha mlemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amejeruhiwa kwenye mzozo wa gerezani, chini ya wiki mbili baada ya kifungo cha kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kuongezwa zaidi ya mara mbili.

Inadaiwa kuwa mwariadha huyo alikuwa kwenye vita vya kupigania simu kwa mujibu wa msemaji wa idara ya mahakama.
Pistorius ambaye amefungwa miaka 13 na miezi mitano aliripotiwa kupata jeraha.
Hakuna majeraha mengine yaliripotiwa.
Inaripotiwa kuwa alikuwa kwenye majibizano na mfungwa mwingine kuhusu kuitumia simu ya umma katika kituo ambapo wafungwa hao wote wamefungwa.
Idara ya mahakama imeanzisha uchunguzi kujua ukweli na kuchukua hatua zinazohitajika.
Kisa hicho kilitokea tarehe 6 mwezi Disemba.
Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia, baada ya kudai kuwa alimpinga risasi Bi Steenkanp akidhani kuwa ni jambazi mapema siku ya wapendanao mwaka 2013.
Lakini mahakama ya rufaa ilibatilishwa uamuzi huo mwaka 2015 na kumpata na hatia ya kuua.
Pistorius alikatwa miguu yake yote miwili akiwa mtoto.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!