Monday, 11 December 2017

NAFASI ZA KAZI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU - WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI OSHA, TUMA MAOMBI KABLA YA TAREHE 29 DECEMBER 2017

Image result for job vacancies
NAFASI ZA KAZI  OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU - WAKALA WA USALAMA NA AFYA  MAHALI PA KAZI OSHA
 
Wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi ni taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa sheria ya wakala wa Serikali namba 30 ya mwaka 1997 ambayo majukumu yake yameidhinishwa katika sheria ya usalama na afya mahala pa kazi namba 5 ya mwaka 2003. Wakala pamoja na kazi nyingine una dhamana ya kusimamia usalama na afya za wafanyakazi waanapokuwa kazini
 
Ili kuhakikisha  kuwa wakala unatekeleza majukumu kama ilvyoidhinishwa katika sheria tajwa hapo juu mtendaji Mkuu anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zipatazo kumi na 6 za kada tofauti kama ifuatavyo
 
1. DEREVA II NAFASI 10
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na cheti cha kidato cha 4 
- awe na leseni ya daraja E au C1 ya uendeshaji wa magari
- awe na uzoefu wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali
- awe amehudhuria  mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari yanayotolewa na chuo cha mafunzo cha stadi VETA AU chuo kingine kinachotambulika na Serikali
- Waombaji wenye vyeti vya majaribio ya ufundi daraja la II watanza kufikiriwa
 
MAJUKUMU YA KAZI 
 
i/ kukaguaa gari kabla na baada  ya safari  ili kubaini hali ya usalama wa gar
ii/ kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbli kwenye safari za kikazi
iii/ kufanya mategenezo madogo madogo ya gari
iv/ kukusanya na kusambaz nyaraka mbali mbali
v/ kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
vi/ kufanya usafai wa gari
vii/ kufanya kazi nyingine kadri atakavyo pangia na msimamizi wake
 
MSHARA 
OSHA 3.1 kwa mwezi
 
MTUNZA KUMBU KUMBU MSAIDIZI  NAFASI 4
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
- awe amehitimu mafunzo ya utunzaji kumbu kumbu katikka ngazi ya cheti  katka moja wap ya fani ya masijala  kutoka katika vyuo vinavyotambulika na serikali
 
MAJUKUMU NA KAZI 
i/   kutafuta kumbu kumbu, nyaraka na majalada yanayohitajiwa
ii/ kuthibiti upokeaji na uandikishaji a kumbu kumbu 
iii/ kuchambua , kuorodheshana kupanga kumbukumbu
iv/ kufungua majalada mapya yanayo hitajika
v/ kuweka kumbukumbu katika majalada, makabati reki katika masijala
vi/ kuthibitisha machapisho kwaajili ya kumbukumbu za ofisi ndani ya muda uliopngwa
vii/ kutoa elimu ya mar kwa mara kwa maafisa wanao kiuka utaratibu was uhifadhi wa kumbu kumbu
viii/ kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na msimamizi
 
MSHARA
OSHA 4.1 Kwa mwezi
 
MHASIBU MSAIDIZI NAFASI 4 
 
SIFA ZA MWOMBAJI
- awe na stashahada ya kawaida ya uhasibu  kutoka chuo/taasisi yoyote inayotambulika na serikali
- awe na cheti cha ufahulu wa mtihani mgumu wa uhasibu serikalini  (higher standard government accountacy examination) unaotelewa na chuo cha utumishi wa Umma
- awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja katika fani ya ushasibu
 
MAJUKUMU YA KAZI
i/ kupokea na kulpa fedha
ii/ kutunza dftari la fedha
iii/ kufanya suluhisho la hesabu za benki (bank reconciliation)
iv/ kukagua hati za malipo
v/kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
vi/ kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
vii/ kufanya kazi nyingine atakayo pangiwea na msimamizi wake
 
MSHARA 
OSHA 4.1 kwa mwezi
 
MASHARTI KWA UJUMLA
- waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri wa miaka isiyozid 45
- waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
- waombaji waambatanishe maelezo binfsi yanayojitosheleza yenye anwani na namba za simu pamoja na  majina ya wadhamini wa 3
- maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakla za vyeti vya kidato cha 4 na 6 kwa wale walifika kidato cha 6
- waombaji waliosoma nje ya Tanzania  wakikishe vyeti vyao  vimehakikiwa na kudhibitiswha na mamlaka husika (TC/NECTA)
- WATAKAO WASLISHA TAARIFA ZA UONGO WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
- Maombi yatumwe kwa njia ya posta au kwa mkono  kufikishwa  ofisi za makao makuu zilizopo kinondoni bara bara ya mahakama
- mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29/12/2017
- maombi yatakayao wasilishwa nje ya utaratibu hayatafanyiwa kazi
 
Jinsi ya kutuma maombi
 
Maombi yatumwe kwa
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI,
S.L.P 519,
DAR ES SALAAM
 
SOURCE MWANANCHI DECEMBER 11 2017

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!