Monday, 11 December 2017

MASHUJAA WETU WALIOPOTEZA MAISHA *DEDICATION POEM FOR JWTZ*


Tunalala kwenye vumbi na matope ili wewe ulale kitandani,
Tunala na bunduki ili wewe ulale na mwenzi wako,
Tunalala porini ili wewe ulale kwenye nyumba,


Unavaa kofia maridadi ya kupendeza,
Sisi tunavaa kofia ngumu na nzito za chuma,
Unavaa "vest" nzuri ya pamba, sisi tunavaa "vest" za shaba,
Unavaa mkanda wa ngozi kiunoni, sisi tunavaa mikanda ya risasi,
Asubuhi unaamshwa na "alarm" nzuri ya simu yako,
Sisi tunaamshwa na milio ya mabomu na risasi,
Unatembelea gari zuri la thamani,
Sisi tunatembelea vifaru na malori,
Unakula chakula kizuri ukipendacho,
Tunakula wadudu na matunda porini,
Tunakesha ili wewe upate usingizi,
Tunaua ili wewe uishi,
Tunaumia ili wewe upone,
Tunaitoa sadaka "leo yetu" kwa manufaa ya "kesho yako",
Tunatoa sadaka maisha yetu ili kutetea maisha yako,
Tunakupigania usiku na mchana kwa sababu tunakupenda,
Tunaipenda nchi yetu,
Sisi ni wanajeshi,
Sisi ni wazalendo,
Sisi ni mashujaa,
Ombea wote waliofia vitani,
Wamekufa nchi yetu,
Wamekufa wakitetea uhai wako,
Ni mashujaa wetu,
Nchi yetu,
Amani yetu,
Jeshi letu.
MUNGU LIBARIKI Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ)!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!