SERIKALI imetakiwa kuendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili visiathiri malezi hayo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Dodoma, yaliyofanyika katika kijiji cha Mlowa barabarani, mwanafunzi Eunice Mwaipopo alisema watoto wamekuwa wakikabiliwa na ukatili ambao wakati mwingine umekuwa ukiathiri maendeleo yao shuleni. “Watoto wamekuwa wakikabiliwa na adhabu kali majumbani, kuachishwa shule na hata mimba za utotoni,” alisema.
Alisema jamii ina wajibu wa kuhakikisha watoto wanalindwa na haki zao zinaheshimiwa. Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Yohana Magomba alitaka hatua stahiki ziwe zinachukuliwa kwa wote wanaofanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
“Hapa kijijini kuna mtoto alifanyiwa ukatili na mlezi wake, alipigwa, akafungwa kamba na kutishiwa kuuawa kabla ya kupandishwa na kuning’inizwa juu ya mti, baadaye mwanamke aliyefanya ukatili huo alikamatwa lakini tukashangaa baada ya siku chache akarudi kijijini,” alisema. Alisema vitendo vya rushwa vimekuwa vikisababisha matukio mengi ya ukatili kuishia juu juu licha ya taarifa kutolewa na wahusika kukamatwa lakini hakuna adhabu yoyote wanayopewa
No comments:
Post a Comment