Wednesday, 15 November 2017

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB)

[​IMG]
Kifua kikuu(TB )ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria anaejulikana kwa jina la Mycobacterium tuberculosis



Mycobacterium tuberculosis ni aina ya bacteria anaesababisha TB kwa binadamu ingawa zipo jamii zingine za Mycobacterium zinazoweza pia kusababisha TB kwa binadamu. Bacteria huyu anaweza kuingia kwa binadamu na kusababisha TB katika mfumo wowote wa binadamu. Mfano mtu anaweza kuwa na TB ya mapafu, figo, ktk mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ktk ngozi, ubongo nk….

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchini Tanzania ugonjwa wa Kifua Kikuu umekuwa ukiongezeka kwa kasi kubwa ambapo watu elfu 65,000 hivi sasa wanaugua kifua kikuu nchini humo. Kati yao asilimia 50 pia wana ukimwi.

JINSI YA KUENEA

1. Njia kuu ya kuenea ni kwa Kuvuta hewa yenye wadudu hao. Hii ni kutokana aidha na kuishi au kuwa karibu na mtu mwenye ugonjwa huo. Na mara anapopiga chafya au kukohoa bila kufunika mdomo ndipo wadudu hao wanaweza kukupata.

2. Kula vyakula visivyopikwa vikaiva vizuri. Kuna jamii ya watu wanaokunywa maziwa ambayo hayajachemshwa pia wako ktk hatari ya kupata bacteria hao.

NANI YUKO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA TB?

Kundi ambalo liko kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa Tb au kifua kikuu ni la wale wanaoishi kwa karibu na kwa muda mrefu na mtu yule aliyekwisha ambukizwa ugonjwa huo ambae bado hajaanza matibabu (kumbuka kuwa, mara baada ya mgonjwa wa TB kuanza matibabu, baada ya wiki 1 ya matibabu anakuwa hawezi kusambaza TB)! Nitaorodhesha makundi ambayo yako kwenye hatari na ya uwezekano mkubwa wa kuambukizwa Tb iwapo watakuwa karibu na mgonjwa. Watu hawa ni rahisi kupatwa na kifua kikuu kwa sababu kinga zao za mwili huwa ni za kiwango chini: Watoto wadogo na wazee, wale wote wanaougua kisukari, watu wnaotumia dawa aina ya steroids au dawa nyinginezo zinazoathiri mfumo wa kinga ya mwili, waathirika wa ukimwi na HIV, wale wote wanaoishi maeneo yenye msongamano mkubwa watu yaliyoduni kiafya, wanaoishi kwenye sehemu zisizokuwa na hewa ya kutosha, watu wanaotumia dawa mbalimbali, au pombe na mwisho wale wenye lishe duni.

DALILI ZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

1. Kikohozi cha muda mrefu (wiki mbili au zaidi)

2. Kukohoa damu

3. Homa isiyoisha-hasa homa ambayo inapanda sana wakati wa usiku; ikiambatana na kutoka jasho jingi wakati wa usk=iku kiasi cha kulowesha mashuka.

4. Kupungua uzito kusiko kawaida

5. Na pia maumivu ya kifua wakati wa kukohoa.

6. Dalili zingine ni kupungua hamu ya kula,kuchoka na kutoka jasho wakati wa usiku.

NAMNA YA KUZUIA

1. Kama tayari umeambukizwa TB, hakikisha unapokohoa au kupiga chafya unafunika mdomo wako ili kuepuka kumuambukiza mwingine.

2. Unapotema mate hakikisha unayafukia vizuri

3. Unapoishi na mtu mwenye ugonjwa wa TB hakikisha unamsisitiza kuwa aende hospitali kupata matibabu mapema.

4. Nenda hospitali mara unapokua na dalili zinazofanana na hizo hapo juu ili kujihakikishia afya yako na kuanza tiba mapema kabla hujasambaza kwa watu wengine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!