Sunday, 15 October 2017

Wanandoa wauawa kwa mapanga

WANANDOA wakazi wa kitongoji cha Kasekese “B”, Kata ya Kasekese wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi, Adamu Charles Mtambo (41) na mkewe Catharina Gabriel (39) wameuawa baada ya kushambuliwa na mapanga usiku wa kuamkia jana.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kasekese, Happiness Bona alisema wanandoa hao walipoteza maisha, wakati wakazi wa kijiji hicho wakiwa katika harakati za kusaka gari la kuwasafirisha kwenda Hospitali ya Wilaya ya Mpanda mjini Mpanda kwa matibabu.
Aidha watoto watatu wa wanandoa hao walijeruhiwa kwa kucharazwa fimbo walipoingia chumbani kwa wazazi wao ili kuwazuia wasiuawe na watuhumiwa hao. Mtambo ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka mawili.
Mauaji haya yametokea siku tatu baada ya mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji mikoa ya Rukwa na Katavi (CCWT), Suzane Charles (40) kuuawa kwa kupigwa risasi tano kifuani akiwa nyumbani kwake kitongoji cha Msikitini katika kijiji cha Kapanga kilichopo katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema wanaendesha msako kusaka wauaji hao.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!