Sunday, 15 October 2017

Vyakula na matunda vyenye uwezo wa kupunguza uchovu


Ni wazi kwamba kuna wakati huwa tunajikuta tumezongwa na uchovu sana huenda kutokana na shughuli zetu za kimaisha na hasa zile za kujiongezea kipato.


Miongoni mwa dalili za tatizo hili la uchovu ni pamoja na kupatwa na maumivu ya misuli, kukosa hamasa ya kufanya kitu chochote, kupoteza umakini na hata kupotea kwa hamu ya kula pia.

Kwa mujibu wa taasisi iitwayo National Institutes of  Health iliyopo nchini Marekani inakadiria kwamba mtu mmoja kati ya watano nchini Marekani hukabiliwa na tatizo la uchovu katika maisha yao, huku wakibainisha kwamba mara nyingi tatizo hili huwakumba zaidia wanawake kuliko wanaume.

Lakini hakuna mtu anayependa kuishi akiwa mchovu wa mwili siku zote, kutokana na hali hiyo hapa napenda kukufahamisha baadhi ya vyakula vyenye uwezo wa kuondosha uchovu wa mwili.


Mbegu za maboga
Hizi nazo ni nzuri kwa kuondoa uchovu kwani ndani yake mhusika hupata protini pamoja na vitamin B1, B2, B5 and B6, sambamba na madini kama manganese, magnesium, phosphorus, iron na copper. Virutubisho vyote hivyo kwa pamoja husaidia sana kuimarisha kinga za mwili na kuupatia mwili nguvu ya kupambana na hali ya uchovu.


Maziwa mtindi.
Maziwa mtindi yana kiwango kikubwa cha protini, carbohydrates, hivyo maziwa mtindi kutokana na kuwa na virutubishi hivyo yanaingia kataka nafasi ya kuwa na uwezo wa kupambana na shida ya kuchoa mwili


Ndizi mbivu
Tunda hili ndani yake lina madini ya potassium ambayo ni muhimu kwa mwili kwani husaidia ubadilishaji wa sukari kuwa chanzo cha nishati au nguvu mwilini, lakini pia ndizi ndani yake zinautajiri wa vitamin B, vitamin C, nyuzinyuzi 'fiber' karbohydrates, ambavyo kwa pamoja huwa na nafasi ya kuondosha dalili za kuchoka choka kwa mwili na kumfanya mhusika kujihisi vizuri


Tikiti maji
Tunda hili nalo linauwezo wa kumaliza haya matatizo ya uchovu wa mwili

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!