Thursday 19 October 2017

Mamake mwanajeshi wa Marekani asema Trump hakuwa na huruma

Mjane wa mwanajeshi aliyeuawa akibubujikwa na machozi katika jeneza la mumewe

Haki miliki ya pichaCBS
Image captionMjane wa mwanajeshi aliyeuawa akibubujikwa na machozi katika jeneza la mumewe

Rais wa Marekani Donald Trump amejipata mashakani kwa mara nyingine kuhusiana na kauli yake aliyoitoa kwa mjane wa mwanajeshi wa nchi hiyo aliyeuawa vitani nchini Niger.

Rais Trump amekana tuhuma kuwa alimwambia mjane wa mwanajeshi huyo kuwa mumewe alikuwa anajua kile alichoweka saini kwa kazi anayoijua hatma yake.
Mamake mwanajeshi huyo ambaye aliuawa wakati wa vita ameunga mkono madai ya bunge la Congress kwamba rais Trump hakuwa na huruma wakati wa mawasiliano ya simu na mkewe mwanawe marehemu.
Mbunge Federica Wilson alisema kuwa alimwambia Myeshia Johnson : Alijua alichokuwa ametia saini , ''lakini nadhani ni uchungu bila shaka''.
Bwana Trump anasema kuwa madai hayo yalitungwa.
Sajenti La David Johnson aliuawa nchini Niger na wapiganaji wa kiislamu mwezi huu.
Alikuwa mmoja wa wanajeshi maalum waliouawa baada ya kuvamiwa.


Bwana Trump alikuwa tayari amekosolewa kwa kutowasiliana na familia za wanajeshi waliouawa muda mfupi baada ya shambulio hilo la terehe 4 mwezi Oktoba.
Mamake sajenti Johnson , Cowanda Jones-Johnson aliunga mkono kauli ya mbunge Wilson kuhusu mazungumzo hayo ya simu.
Rais Trump hakumuheshimu mwanangu na mkewe pamoja nami na mume wangu , aliambia gazeti la The Washington post.
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!