Thursday, 5 October 2017

Diamond afunguliwa kesi ya udhalilishaji


Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa mahakama ya watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.




KISUTU, DAR: Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia kesi ya madai mzazi mwenzie, Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi kwa udhalilishaji pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao, Abdul Naseeb Juma.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Hamisa Mobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
- Shauri hilo linatarajiwa kutajwa ifikapo Oktoba 30, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!