Sunday, 1 October 2017

Acheni kunyanyasa wazee nchini-Tume


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa mwito kwa jamii kuondoa vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wazee.


Mwito huo ulitolewa jana jijjini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Iddi Mapuri ikiwa ni salamu za Tume katika maadhimisho ya Siku ya Wazee, yanayofanyika duniani kote leo. Kauli mbiu ya siku hii kitaifa ni ‘Kuelekea uchumi wa viwanda:Tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.’
Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, THBUB, ilisema hatua ya uzee na kuzeeka havikwepeki hivyo jamii na serikali inapaswa kuweka mifumo madhubuti ya kulinda na kutetea haki za makundi maalum yanayohitaji ulinzi wa jamii husika. Alisema ni kupitia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Desemba 14, mwaka 1990 ,katika Azimio lake Na. 45/106 ulipitisha tarehe 01 Oktoba, ya kila mwaka kuwa siku ya wazee Duniani.
Vipaumbele katika Azimio hilo ni pamoja na suala la uhuru wa wazee, wazee kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za maendeleo, kutunzwa na kuheshimiwa na kwamba siku hiyo pia hutumiwa na wazee kukutana pamoja na kubadilishana nawazo ya kuleta maendeleo ya taifa.
Mapuri alisema Tanzania ni moja ya nchi zilizosaini kutambua, kulinda na kutetea haki za wazee na kwamba THBUB nayo inatambua na kuzilinda na kuitaka jamii kujenga tabia hiyo kwa makundi kama hayo. Pamoja na kulinda haki hizo, Mapuri alisema bado kuna changamoto katika jamii ambapo wazee bado wengi wao wanauawa kwa tuhuma za ushirikina.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!