Saturday 9 September 2017

Watu 11 Wakamatwa wakiandamana Kupinga Lissu Kupigwa Risasi


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu amesema watu hao wamekamatwa na polisi jana Ijumaa mchana wakiwa na mabango katikati ya mji wa Ikungi, wakiwa kwenye harakati za kuhamasisha maandamano.



Watu 11 wakiwemo madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya IKungi mkoani Singida wamekamatwa wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuishinikiza Serikali kutoa tamko kuhusu kuvamiwa na kupigwa risasi mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.

“Walitaka kufanya maandamano, tuliwawahi kabla hawajaanza, miongoni mwao wapo waliotokea Arusha na Dodoma, kwa hiyo wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi,” amesema Mtaturu.
Amesema tukio la Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi halijatokea Singida, hivyo hawataruhusu maandamano ya aina yoyote yanayoweza kuhatarisha amani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!