Sunday, 24 September 2017

Walionusurika ajali Uganda kurejea kesho


MAJERUHI watano walionusurika kwenye ajali ya gari iliyopoteza maisha ya Watanzania 13 nchini Uganda mapema wiki hii wanarejea kesho.


Majeruhi hao walihusika kwenye ajali ya gari iliyohusisha basi dogo la kukodi aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 540 DLC wakati wakitokea nchini Uganda kuhudhiria harusi ya daktari binti wa Kitanzania, Dk Annette Teu na mumewe Dk Treausuer Ibingira ambaye ni raia wa Uganda.
Baada ya ajali hiyo Watanzania hao watano walilazwa kwenye Hospitali ya Nsambya iliyopo jijini Kampala ambapo juzi jioni waliruhusiwa kutoka hospitalini hapo. Akizungumza na Gazeti hili kwa njia ya simu kutokea jijini Kampala, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgovano alifafanua kuwa walifikia nyumbani kwake na kwa sasa wanajiandaa kwa safari yao hiyo ya kesho.
Alisema, wanaendelea vema na wamepata ahueni kubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa mwanzo na kuongeza kuwa wakiwasili Dar es Salaam wataendelea na taratibu za kuonana na madaktari kwa uangalizi wa kawaida. Grace aliwataja Watanzania hao kuwa ni Erasto Teu, Esther Alex, Severia Sanga, Irene Lyatuu na Dativa Shayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!