Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu),
Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready
Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi,
Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme
vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la
Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo
ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali
nchini.
NA
MWANDISHI WETU SONGEA.
KAMPENI
ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti
16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani, amezindua mradi huo kwenye
kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa
vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.
Katika
hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista
Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja
bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).
“Kifaa
hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji
analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja
Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye
ziara hiyo.
Hali
kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO
za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.
Alisema,
tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya
Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.
“Jambo
la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali
yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)”
alifafanua Bi. Muhaji.
No comments:
Post a Comment