Thursday, 3 August 2017

Marubani wafukuzwa kazi baada ya kuruhusu mtoto kuendesha ndege

Marubani wafukuzwa kazi baada ya kuruhusu mtoto kuendesha ndege
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarubani wafukuzwa kazi baada ya kuruhusu mtoto kuendesha ndege
Marubani wawili wanaofanya kazi na shirjka la ndege la serikali nchini Algeria wamefukuzwa kazi baada ya kumruhusu mtoto yatima mwenye umri wa miaka kumi kuendesha ndege ya abiria.

Mtandao wa Africa News unasema kuwa zoezi hilo liifadhiliwa na kurekodiwa na runinga ya El Bilad TV, waliomuonyesha mtoto huyo akiwa amavaa sare za rubani akibofya vitufe katika chumba cha rubani.
Haijulikani ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Air Algerie kutoka mji wa Algiers hadi mji Setif.
Mtandao huo unasema kuwa rubani hao walifukuzwa tarehe 29 mwezi Julai huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa sababu kitendo hicho kilikiuka sheria za usafiri wa ndege.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!