Tuesday 4 April 2017

Makamishna Uhamiaji wapanguliwa


Dar es Salaam. Panguapangua imeikumba Idara ya Uhamiaji baada ya makamishna na naibu makamishna kuteuliwa kuwa wakuu wa uhamiaji wa mikoa, huku wengine wakihamishwa vituo vya kazi.

Akitangaza mabadiliko hayo jana, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makalala alisema Naibu Kamishna Sixtus Nyaki, aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa Simiyu, wakati aliyekuwa Rukwa, Selemani Kameya amehamishiwa Tabora.
Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Asumsio Achacha amehamishiwa Kaskazini Pemba na wa Manyara, Peter Kundy amehamishiwa Dodoma kuchukua nafasi ya Alli Mohamed aliyehamishiwa Arusha.
Katika mabadiliko hayo, Naibu Kamishna Mkemi Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kusini Unguja na Naibu Kamishna, Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kaskazini Unguja.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!