Wednesday, 21 December 2016

Maafisa wa Nigeria wamekamata mchele wa plastiki


Image captionUchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemsha, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya wali wa kawaida
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.


Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".
Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!