Tuesday, 8 November 2016

NGE



Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na buibui na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu. Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. 


Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia. Kama unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au kama baada ya kuuma kuna dalili za matatizo kama vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na buibui na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi  dawa ya diazimu  kuzuia misuli kukakamaa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.

Via-Hisperian Health guides

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!