Sunday 30 October 2016

NEWZ ALERT:BASI LA SAFARI NJEMA LILILOKUWA LIKITOKEA DODOMA KUJA DAR LIMETEKETEA KWA MOTO KIMARA STOP OVER JIONI YA LEO




Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.


 Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto . 
 Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa
 Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
 Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza
 Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto


Habari na picha kwa Hisani ya Michuzi Jr blog.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!