Mkuu wa polisi Tulsa katika jimbo la Oklahoma Marekani anasema mwanamume aliyepigwa risasi na kuuawa na maafisa Ijumaa hakujihami.
Maafisa wanachunguza kifo cha Terence Crutcher, mwenye umri wa miaka 40, aliyeinusha mikono juu hewani alipopigwa risasi karibu na gari lake, familia yake inasema.
Polisi wametoa kanda ya video ya kamera ya gari iliyonasa mauaji hayo.
Katika video hiyo, anaonekana akiwaondokea maafisa wa polisi na kuelekea kwenye gari lake mikoni ikiwa juu hewani, kabla ya kufika kwenye mlango wa gari upande wa dereva.
Hapo anaanguka chini baada ya kuchomwa na nyaya za umeme kwa kifaa maalum na baadaye akapigwa risasi na kuuawa.
Alifariki hospitalini, polisi wanasema.
Video hiyo pamoja na nyengine kutoka kamera kwenye helikopta ya polisi zinaonekna kuunga mkono inachosema familia yake kuwa mikono yake ilikuwa juu hewani wakati wote.
Maafisa walilipata gari la bwana Crutcher limesimama wakati walipokuwa kazini, taarifa zinaeleza.
Polisi wanasema alikataa kufuata maagizo.
Pacha wa bwana Crutcher, Tiffany ameitisha maandamano kualamikia mauaji na anataka maafisa waliomuua wafunguliwe mashtaka ya uhalifu.
Visa kadhaa vya kuuawa kwa raia wa Marekani wenye asili ya Kiafrika mikononi mwa maafisa wa polisi vimesababisha maandamano kote Marekani.
BBC
No comments:
Post a Comment