Friday, 19 August 2016

Mwingereza afutiwa umiliki ardhi nchini

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 2,188 mkoani Kagera iliyokuwa ikimilikiwa na mwekezaji mwenye Kampuni ya Rockshield Quality Food Processors Ltd ya Uingereza baada ya kuonekana kutofuata taratibu za umiliki kama sheria ya ardhi inavyotaka.


“Kwa mamlaka niliyopewa kutokana na umiliki wako kutofuata sheria na taratibu za ardhi, nafuta umiliki wa ardhi hiyo, kwa hiyo nakuagiza Kamishina Msaidizi wa Kanda ya Ziwa, Joseph Shewiyo ndani ya wiki moja ardhi hiyo aliyokuwa anamiliki George Rogas kurudishwa kama ilivyokuwa zamani. Pia wewe mwekezaji ukitaka kuwekeza tunakukaribisha na ufuate sheria,” ameagiza Lukuvi.
Uamuzi huo umekuja baada ya wananchi wa kata ya Nyanga katika Manispaa ya Bukoba kulalamikia kuvamiwa na mwekezaji huyo raia wa Uingereza, George Rogas anayedaiwa kuwanyanyasa na kuwapiga, kisha kuvamia maeneo yao ya makazi tofauti na ardhi ya ekari tano alizomilikishwa kihalali na manispaa hiyo.
Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Deodatus Balile alisema kata hiyo yenye vijiji vitatu ina ekari 1,863, lakini jambo la kushangaza mwekezaji huyo anadaiwa amejimilikisha ekari 2,119 ambazo ni mali ya wananchi wa kata hiyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!