Mtu mmoja amefariki dunia leo baada ya kugongwa na treni wakati akijaribu kuidandia ikiwa katika mwendo eneo la Kamata jijini Dar
- Alidandia treni hiyo wakati ikiwa Kamata Kariakoo kwenda Stesheni akiwa na lengo la kugeuza nalo kwenda Pugu.
Treni inayotoka Stesheni ya Posta kwenda Pugu mida ya saa 12 jioni, iimesababisha mtu mmoja kufariki baada ya huyo mtu aliye dandia treni na kudondoka chini wakati likiwa katika mwendo. Kijana huyo ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja alidandia treni hiyo Wakati ikiwa Kamata Kariakoo kwenda Stesheni akiwa na lengo la kugeuza nalo kwenda Pugu.
Ndipo akalidandia likiwa kwenye mwendo huku milango ya treni ikiwa haijafunguliwa huku akiwa ananing’inia kwa nje ndipo alipojibamiza kwenye kingo za treni na kudondoka chini.
Ndipo akalidandia likiwa kwenye mwendo huku milango ya treni ikiwa haijafunguliwa huku akiwa ananing’inia kwa nje ndipo alipojibamiza kwenye kingo za treni na kudondoka chini.
No comments:
Post a Comment