Thursday, 4 August 2016

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UJAUZITO




Kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi yanatokea kwenye mwili wa mama na kufanya mabadiliko ya mwili wake kwa  kipindi cha miezi 9. mara  nyingi kuwa  na hali tofauti kama kutapika, kichefuchefu, na kujisikia mwili umechoka na pia uvimbaji wa miguu au uso n.k
















: Lishe ( vyakula muhimu wakati wa ujauzito:

Mama hawezi kuzaa mtoto mwenye afya nzuri bila kula lishe bora, mama mjamzito lazima ale chakula chenye virutubisho mbalimbali vitakavyo mpa nguvu na afya kwake na mtoto.
kula matunda ya kutosha, mboga mbaoga za kijani, mafuta na protein ipatikanayo kwa wanyama kama samaki ,kuku  na nyama, kula vyakula jamii ya mbegu( maharagwe, njegere, kunde choroko  mbaazi n.k

Mayai, maziwa jibini( cheese), mtindi, maboga viazi, mihogo magimbi, ugali wali na mkate, vyote hivyo vinatakiwa ule ili kukuza mtoto  na afya yako.



: Unywaji wa maji kwa wigi.

Mama mjamzito anatakiwa kunywa maji mengi wakati wa mimba ili  kumsaidia kutoa sumu mwilini na kutegeneza maji maji ya amniotic fluid kuwa ya kutosha, yanayohitajika kwa ukuaji vizuri wa mtoto tumboni kwa mama.
Kunywa maji humkinga mama mjamzito na magonjwa ya njia ya mkojo, kwani mama  mjamzito hupatwa na  magonjwa ya njia ya mkojo kwa urahisi sana kipidi cha ujauzito, hivyo maji kwa wingi huondoa hatari ya mama kupata UTI.
Maji pia hufaya gozi ya mama kuwa nyororo na kuvutia, kunywa glasi 7-8 za maji kwa siku itasaidia kuepuka kupata strech marks( michirizi)



: Tunza ngozi yako

Kutokana  na mabadiliko ya mwili hormoni kuchangia mabadiliko a ngozi ya mwanamke kupata chunusi au mabaka meusi  usoni au kifuani. Ni mihimu kuzingatia usafi wa ngozi yako na kuifaya ionekane nadhifu kwa kutumia vitu asilia kama asali ndimu ukichanganya ukapaka usoni mara 2 kwa siku au utomvu wa aloe vera ikatokea mama anapata chunusi nyingi. Mama mjamzito kupata michirizi tumboni kipindi cha ujauzito kinachotakiwa paka mafuta mengi tumboni, mafuta kama (cocoa butter, mafuta ya nazi au palmer oil) inasaidia sana. Kuepuka michirizi usikune tumbo likiwasha bali paka mafuta kwa wingi, fayia masaji hapo utaepuka kupata michirizi (strech marks)



Fanya mazoezi:

Ni muhimu kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ya aina mbalimbali ambayo ni mepesi na hayatokuwa na madhara kwa mtoto.


  • mazoezi kama kutembea kwa mwendo wa dk 20-30 asubuhi na jioni.
  • mazoezi ya kunyoosha mwili( streching) au Yoga.
  • mazoezi ya kuogelea
  • ufanyaji mazoezi humsaidia mama mwili usichoke
  • humsaidia mama kujifungua kwa urahisi
  • Mzunguko wa damu huwa mzuri
  • husaidia kupuguza uzito( unene ) kwa urahisi.
  • kuodoa uchovu mwilini 




  • Utakapo ona dalili au mabadiliko yoyote usio yaeleawa mwilini mwako wahi hospitali.
Mama unaweza tokwa na damu nyingi , maumivu makali chini ya kitovu, pressure kupanda ghafa, kupata homa kali, kuvimba miguu na mikono, kizunguzungu, mtoto kutocheza zaidi ya masaa 48  na dalili nyingine nyingi hatarishi,Wahi hospitali.


:Mavazi

Mama mjamzito anapaswa zingatia kuvaa mavazi mazuri enye kusitiri mwili. Uvaaji wa nguo za kubana sio mzuri utakuwa unakufanya uchoke zaidi na kutokuwa comfort. 

Viatu virefu sio vizuri kwa mama mjamzito kwani huhatarisha maisha ya mama na mtoto, mama mjamzito anaweza kuanguka au kujikwaa ikakusababishia kuanguka na kufikia tumbo na ukaharibu mimba na hata kusababisha kifo kwa mtoto tumboni.



Uzito mkubwa( unene) 

Mama anatakiwa uhakiki uzito wake kipindi cha ujauzito sababu uzito mkubwa ni hatari sana kwa mama na mtoto, hivyo zingatia kupima uzito wako mara kwa mara uendapo klinik iwapo uzito wako utakuwa mkubwa utahitaji kuanza diet.


Epuka matumizi ya pombe na madawa ya kulevya( mihadharati)
Unywaji wa pombe na matumizi ya madawa a kulevya, au sigara ni hatari kwa mama na mtoto, unaweza msabibishia kifo ulemavu, afya dhoofu, ukamzaa mtoto njiti, na pia huweza kuathiri organs za mtoto n.k


  • Jipe muda wa kutosha wa kujipumzisha( kulala)

Urembo:

Suala la urembo nalo ni muhimu kuzingatia usiweze kupoteza urembo wako na usafi. Mimba inapendeza pale mama  anapoonekana msafi na nadhifu, ukiwa kazini au nyumbani. Kwa mama wa nyumbani baadhi wanajiachia sana, sio vizuri haipendezi kutojali  mwili wako, kuna wengine hawataki hata kuoga wala kupiga mswaki jitahidi kuwa msafi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!