Arusha. Mahakama ya rufaa amemuondolea adhabu ya kunyongwa, Nicodemu Daudi(32) ambaye alitiwa hatiani kwa kuwaua watu wawili kwa shoka wakati alipokuwa akigomabana nao kuwadai ujira wa Sh 50,000 .
Majaji ya mahakama ya rufani, Jaji Salum Masati, Jaji Angela Kileo na Jaji Edward Rutakangwa baada ya kutengua adhabu ya kifo walimtia hatiani mtumiwa huyo kwa kuua bila kukusudia na kuamuru atumikie kifungo cha miaka 7 jela.
Jaji Kileo akisoma hukumu hiyo amesema mahakama ya rufani imekubaliana na rufani na mtuhumiwa huyo, kuwa aliua bila kukusudia kutokana na mazingira ya kosa la mauwaji hayo.
No comments:
Post a Comment