Thursday 4 August 2016

DIAMOND-"WATU HAWA WAWILI NDIO NINGEPENDA NIKUTANE NAO"



Mwanamuziki Diamond Platnumz Agosti 2 akifanya mahojiano na kituo cha redio ameulizwa kuwa, tayari...


Mwanamuziki Diamond Platnumz Agosti 2 akifanya mahojiano na kituo cha redio ameulizwa kuwa, tayari amefanikiwa kukutana na watu wengi duniani, watu wa tasnia mbalimbali, akipata nafasi ya kukutana na watu wawili Tanzania, Je! atamchagua nani?
Akijibu swali hilo, Diamond ametaja watu wawili na kueleza sababu kwanini anataka kukutana nao, watu hao ni;-
1. Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Alisema, amewahi kukutana naye wakata hajawa Rais, hivyo angependa kukutana nae sasa hivi aone reaction ya Rais kwake kama itakuwa sawa na ile ya wakati wa kampeni au itakuwa ya namna gani.

2. Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Kampuni ya Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa. Alisema anatamani kujua ni namna gani mfanyabiashara huyu anaweza kufanikisha mambo yote anayoyafanya. Alisema Bakhresa ana biashara nyingi, lakini zote zinakwenda vizuri. Diamond alisema licha ya yeye kuwa mwanamuziki lakini pia anapenda kufanya biashara.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!