MOROGORO: Watu 11 wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu
Kuna ajali mbaya iliyotokea wilaya ya KILOSA ikihusisha Bus la kampuni ya OTTA CLASSIC yenye namba DGK T.201 likitokea BUKOBA kuelekea D'SALAAM likigongana na loli la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.-Ajali hiyo imetokea katika eneo la Veta Dakawa
Kuna abiria wamekufa ikiwajumuisha na madereva wote wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine. Miili ya marehemu imekimbizwa na mingine bado inapelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na kwa itifaki ila mahututi wengine wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa la Roman Catholic.
Rai:Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment