Thursday, 28 July 2016

Papa Francis aanguka akiendesha ibada


Papa Francis akisaidiwa kuinuka baada ya

Poland. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameanguka chini wakati akiwa kwenye ibada iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Jasna Gora Monaster kusini mwa Poland.


Akiwa mbele ya madhabahu, kiongozi huyo alishindwa kujizua na kujikuta akiwa chini hali ambayo iliwalazimu wasaidizi wake kumwinua haraka. Tukio hilo
Papa Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga ambalo wakati mwingine husababisha maumivu sehemu za mgongo na kushuka hadi miguuni. Hata hivyo, hakupata madhara yoyote na aliendelea na ibada iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.
Ulinzi umeimarishwa mara dufu nchini Poland kufuatia matukio ya mashambulizi ya mara kwa mara yanayoendelea kushuhudia katika mataifa ya Ulaya. Papa yupo katika ziara maalumu nchini humo na baadaye atasafiri hadi katika mji wa Czestochowa atakokutana na mamia ya mahujaji.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!