Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti jambo ambalo limemsababisha kuishia mikononi mwa sheria
Akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa gari lililotoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza amesema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana na mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.
''Walipanda watu kama nane ambapo dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe, kijana mmoja mwenye umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni 'mpumbavu' mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza, abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke polisi'' Amesema Bwana. Bushagama.
Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi polisi tulipofika pale nikamwambia askari hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema, amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.
Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kutukanwa namna hiyo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni mpumbavu zaidi yao jambo ambalo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha polisi.
Kamada ameongeza kuwa kwa kuwa suala hilo tayari limefikishwa polisi kitakachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani .
EATV
EATV
No comments:
Post a Comment