HIVI sasa kuna tatizo kubwa la uvimbe linalowakabili kinamama duniani na baadhi wanajikuta wanashindwa kushika ujauzito na madhara mengineyo.




Ni kinamama wachache wanaofahamu sababu za wao kusumbuliwa na maradhi hayo ambayo yanajenga picha ya kuwa ni ya kawaida.
Kimsingi, ni maradhi yanayokuwa katika sehemu inayotengeneza homoni ya kuzalisha mayai kwa mwanamke iitwayo ovari.

“Ovari ndiyo chanzo kikubwa cha homoni za kike zinazoongoza ukuaji wa sifa za msichana kama matiti, umbo la mwili na nywele za mwilini. Homoni hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi na mimba,” wataalamu wanafafanua.
Uvimbe unaelezwa kupatikana ndani ya tezi za uzazi za mwanamke na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.
AINA ZA UVIMBE
Wataalam wa uzazi wanasema kuna aina nyingi za uvimbe. Hata hivyo, kuna aina saba ndizo zinazojulikana zaidi na kuzoeleka na wengi.
Aina mojawapo ni inayojitokeza katikati ya mzunguko wa hedhi kwa mwanamke na kusababisha maumivu. Kwa kawaida, dalili zake hupotea baada ya miezi kadhaa.
Pili, ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi.
Uvimbe huo hujitokeza upande mmoja, iwe ama kulia au kushoto.

Tatu ni uvimbe unaotokana na kuvuja damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ile, ambayo imeshajitengeneza tayari na huambatana na maumivu makali upande mmoja wa mwili.
Huo ni uvimbe unaosababisha saratani na huwapata wanawake wenye umri wa kushika mimba. Kwa kawaida, una uwezo wa kukua kufikia ukubwa wa nchi sita.
Inaelezwa kwamba ni uvimbe hatari zaidi, kwani unaweza kukua na kusababisha maumivu makali, huku ukiathiri mzunguko wa damu yanayofika katika sehemu tofauti za tumbo.
Aina ya tano ya uvimbe ni wenye tabia ya kukua zaidi na unazungukwa na mingine midogo na huwa inaonekana kwa wanawake wote, wenye afya njema na wenye matatizo ya homoni.
Sita, ni aina ya uvimbe unaotokana na mishipa midogo inayojaa maji na kusababisha kuvutika. Ni aina ya uvimbe unaokua hata kufikia upana wa nchi 12 au zaidi.
Aina ya mwisho katika orodha hiyo ni uvimbe unaokuwapo kwenye kuta za mfuko wa kizazi kwenye mayai ya mwanamke.
Ni uvimbe unaowaathiri wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito na inaambatana na maumivu makali kwenye nyonga wakati wa hedhi.
Huo ni uvimbe unaonekana kuwa na damu na uvimbe wenyewe unafanana na rangi ya kahawia, ikiwa na ukubwa unaokaribia nchi moja.
CHANZO CHAKE
Ni nini chanzo cha uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke? Kuna sababu nyingi.
Mojawapo ni kwanza ni historia ya awali ya mhusika. Hilo linafanya tatizo lililoko kwenye maisha ya mtu mmoja kuwa na uwezekano kusumbuliwa na ugonjwa huo.
Sababu nyingine inayosababisha uvimbe, mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum au mwili kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili. Ni tatizo linalowapata zaidi wanawake wanene.
Jingine ni ugumba na kuvunja ungo mapema kwa kinamama. Mtoto wa kike anafikia hali hiyo akiwa na umri mdogo.
Aidha, kukosekana uwiano sawa wa vichocheo au homoni na baadhi ya dawa za kutibu saratani nazo zinaelezwa kusababisha tatizo hilo.
DALILI ZA UVIMBE
Sehemu kubwa ya uvimbe huwa hauonyeshi dalil, isipokuwa kwa wachache wakiwa ni kati ya asilimia 15 na 30 ya wanawake wpte wanaipatwa na tatizo hilo.
Dalili mojawapo ya uvimbe ni kutokwa damu kusiko kwa kawaida au kupata damu ya hedhi katika kipindi kisicho cha hedhi.
Namna nyingine ni kwamba mtu anapata maumivu makali wakati wa hedhi na maumivu ya tumbo, kiuno na mgongo.
Kwa baadhi ya wanawake ni kwamba, mtu anahisi au kugusa uvimbe chini ya kitovu na wakati mwingine huvimba na mithili ya ya kuwa na ujauzito.
Ugumba kwa kinamama nayo ni dalili nyingine ya uvimbe, kwa mimba kutoka mara kwa mara wa kushindwa kabisa kushika mimba.
Wakati mwingine mwanamke anapopatwa na haja ndogo mara kwa mara na anashindwa kuzuia mkojo katika hali fulani, anapatwa na maumivu makali wakati wa kufanya mapenzi, kuvimba miguu au kukosa choo ni sehemu ya dalili zake.
Hiyo ni hali inayojitokeza wakati uvimbe unapokandamiza sehemu nyingine ya viungo vya mwili na kusababisha maumivu.
UGUNDUZI WA MATIBABU
Uvimbe katika uzazi hugunduliwa, kutokana na historia ya ugonjwa na vipimo vinavyothibitisha.
Kipimo cha maabara cha ‘Ultrasound’ kinachofanywa tumboni na kwenye kiuno, hutumika kugundua tatizo la uvimbe mahali ilipo na jinsi lilivyo.
Utafiti wa wataalam unabainisha kwamba, Ultra Sound ina uwezo wa kuonyesha ukubwa wa uvimbe, idadi na mahali ilipo na ugunduzi mwingine wa kimaumbile.
Pia kuna kipimo cha ‘Hysterosalpingography’ ambacho hutumika kutafiti kuta za ndani za tumbo la uzazi na kuweza kuonyesha kama uvimbe upo ndani ya tumbo au kwenye mirija ya uzazi.
Kipimo kingine ni aina ya MRI ambayo huonyesha uvimbe ulipo, idadi yake na ukubwa ulio nao.
MATIBABU
Uvimbe katika uzazi unaweza kutibiwa na kupona. Aina ya matibabu inayofanyika hutegemea wingi wa uvimbe, umri wa mwanamke na mambo mengine yanayohusiana na uzazi.
Kuna njia kadhaa zinazoweza kutumika kutibu tatizo hilo. Mojwapo ni upasuaji unaofanyika kwenye tumbo la uzazi na kisha uvimbe huondolewa na kizazi kubakizwa.
Njia hiyo hutoa uwezekano wa kupata ujauzito siku za baadaye kwa mwamamke huyo.
Hata hivyo, ni hali inayoweza kusumbua kupata ujauzito kwa mwanamke kutokana na makovu ya kizazi baada ya uvimbe kuondolewa.
Njia hiyo hutumika zaidi kwa mwanamke mwenye miaka 40 au zaidi na hana nia ya kupata mtoto tena.
Upasuaji hufanyika kwa mfuko kizazi kuondolewai. Baada ya operesheni hiyo, mwanamke hawezi kupata ujauzito tena.
Matibabu mengine ni kwa kuziba mishipa ya damu inayoenda kwenye uvimbe na inatumika
kuziba mishipa ya damu kwenye tumbo la uzazi.

Mishipa hiyo inapozibwa, kiasi cha damu kinachoenda kwenye uvimbe hupungua.
Pia kuna dawa inayoufanya uvimbe kusinyaa na kupunguza ufanyaji kazi wa homoni kwa namna inayopunguza ukuaji uvimbe.
MADHARA
Kwa ujumla, madhara ya jumla uvimbe tumboni kwa mwanamke ni kupata ugumba,mimba kutoka mara kwa mara, upungufu wa damu, kuvuja mkojo na kujifungua
mtoto njiti

Makala hii imaeandaliwa kwa msaada wa taarifa za kitaalamu kuhusu afya