Wakulima Mbarali waanza kunufaika na kilimo cha mpunga
WAKULIMA wa zao la mpunga katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya wameanza kunufaika na kilimo cha zao hilo kwa kutafutia soko la uhakika na pembejeo za kilimo ambazo zimesaidia kuongeza kipato cha wakulima.
Maisha ya wakulima wa Mbarali yameboreshwa kwa kuwa sasa wana uwezo wa kusomesha watoto, kubadilisha milo ya chakula na mahitaji mengine wanayotaka kwa kupata soko la uhakika.
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), ndiyo wadau wa kilimo hicho kwa kutoa msaada kwa wakulima wilayani Mbarali kwa kuwapatia pembejeo za kilimo, soko la kuuzia mazao yao na elimu ya kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu bora.
Akizungumza na Nipashe juzi, Juma Nyasa, ambaye ni mkulima wa zao la mpunga alisema kuwa SNV, limewasaidia kufahamu namna nzuri ya kuandaa shamba kabla na baada ya mavuno ili kuongeza uzalishaji.
Nyasa alisema katika kuboresha kilimo cha mpunga wameshauriwa kutumia mbegu bora zilizo rafiki na mazingira ili kuepuka magonjwa nyemelezi kwa mpunga na magugu mengi shambani.
“Maisha yetu yamekuwa mazuri tangu tupatiwe pembejeo za kilimo pamoja na mbegu bora, tunawashukuru sana wadau wa kilimo kwa kusaidia,” alisema.
Alisema awali walikuwa wanatumia jembe la mkono ambalo kiafya lina athari, lakini tangu pembejeo wapatiwe pamoja na elimu ya kilimo bora, imerahisisha shughuli za kilimo.
Akizungumzia suala la kuwasaidia wakulima wa zao la mpunga, Meneja wa Mradi wa SNV, Erastus Mkojera, alisema wameamua kuwasaidia wakulima wa zao hilo ili kuongeza kipato na uzalishaji.
Mkojera alisema kama wadau wa kilimo, wamewasaidia wakulima kutumia mbinu bora za kilimo ili kuonyesha matokeo mazuri katika uzalishaji.
Alisema, SNV inahudumia wilaya sita katika mikoa ya Rukwa, Mbeya na Songwe, na kuona mwamko mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo baada ya kutumia elimu waliyoitoa.
Alisema kuwa lengo la Shirika hilo ni kuwafikia wakulima wadogo wadogo 45000, kwa sasa wamewafikia wakulima 36000, hivyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kutimiza azma ya kuwasaidia wakulima.
“Hivi sasa tumejikita katika kuwahamasisha wakulima kuendesha kilimo shadidi kutokana na kilimo hicho kuendana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo husababisha mvua kuwa chache hivyo

No comments:
Post a Comment