Friday, 3 June 2016

Hali yazidi kuwa tete kitongoji kulikotokea mauaji ya kinyama



Tanga. Hali imeendelea kuwa tete katika Kitongoji cha Kibatini mkoani Tanga kulikotokea mauaji ya watu wanane waliochinjwa shingo zao.



Wakazi wa eneo hilo wameanza kuyahama makazi yao wakihofia usalama wa maisha yao.
Watu hao walichinjwa usiku wa Mei 31 nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho kwa madai kuwa walisababisha “vijana” wao kukamatwa na polisi baada ya kutoa taarifa zao wakati wakizurura kwenye eneo lao.
Jana baada ya maziko, mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk alipeleka lori aina ya Mitsubishi Fusso kwa ajili ya kuwahamisha wanakijiji hao.
Diwani wa kata ya Mzizima, Fredrick Chiluba alisema wakazi hao wameamua kuhamia kitongoji cha Kona-Z kilichopo kijiji jirani cha Kiomoni.
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!