Thursday, 30 June 2016
MAPISHI YA LEO-KUKU WA NAZI!
MCHUZI WA KUKU WA NAZI
Mahitaji:-
Kuku 1
Viazi mbatata vilivyokatwa 2
Pilipili nyekundu ya unga kjk 1 1/2 chakula
Giligilani ya unga 1-1/2 chakula
Manjano 1/2 kjk chai
Tui la nazi zito kikombe 1 1/2
Tui la nazi jepesi vikombe 2
Vitunguu 2 vilivyokatwa
Tangawizi ilokatwa 1/2 kjk chakula
Kitunguu saumu kilichokatwa
1/2 chakula
Kipande cha mdalasini
Karafuu 2-3
Hiriki 2
Shimari 1/4 kjk chai
Majani ya curry 1
Vitunguu vilivyokaangwa 1/4 kikombe
Mafuta ya kula vjk 4 chakula
Maji kiasi
Chumvi kiasi
MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA
1.Tia sufuria na mafuta vjk 2 jikoni kisha kaanga viungo (giligilani,pilipili ya unga na manjano ) Epua acha vipoe ktk sahani.
2. Tia viungo uloivyokaanga na chumvi ktk kuku, changanya vzr kwa mikono kisha funikia acha ktk fridge kwa muda wa dk 30 kuku aingie viungo.
4. Kaanga viungo vizima kisha saga kufanya powder. Weka pembeni
5. Tia sufuria na mafuta jikoni kaanga vitunguu hadi vilainike, tia tangawizi na saumu kisha kaanga hadi iwe brown kisha tia kuku wako na kaanga kwa dk 5.
6. Punguza moto kisha tia tui jepesi na maji,acha ichemkie ukiwa wakoroga mara kwa mara hadi kuku apate kuiva.
7. Tia viazi pamoja na viungo vizima ulivyosaga na maji kidogo acha ichemke hadi viazi viive.
8. Tia tui zito,onja chumvi kisha acha itokote hadi mchuzi uwe mzito. Epua
9. Tia mafuta yalobaki ktk sufuria jikoni kaanga majani ya curry kidogo kisha mwagia ktk mchuzi wako pamoja na vitunguu vilivyokaangwa, koroga kisha funikia.
SPECIAL THANKS TO MAPISHI MIX
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment