Thursday, 23 June 2016

Diamond: Niombeeni Nirudi na Tuzo


WAKATI akisafiri kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki utoaji wa tuzo za BET, msanii wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’, amewataka Watanzania waendelee kumuombea ili arudi na tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Juni 26.




Diamond alichaguliwa kuwania tuzo hizo kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika (Best International Act Africa).
Kupitia kwa meneja wake, Babu Tale, licha ya Diamond kuwashukuru Watanzania kuendelea kumtia moyo kutokana na kazi zake mbalimbali zinazoendelea kumtangaza kimataifa, ameomba maombi ya Watanzania ili aweze kushinda tuzo hiyo.
“Mniombee ili nirudi na tuzo, naamini Watanzania wananiombea ndiyo maana kazi zangu zinaendelea kufanya vizuri kimataifa naomba muendelee kunitia moyo nirudi na tuzo,” alisema Diamond.
Diamond aliyeshinda tuzo mbalimbali ikiwemo Kili, Afrima na nyingine nyingi alitarajiwa kusafiri kesho kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki utoaji wa tuzo hizo.
Mtanzania

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!